Sunday 9 February 2025 - 10:25
Jumuiya ya Walimu wa Seminari kuunga mkono onyo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu mazungumzo na Marekani

Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom ilisema: Onyo zito la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu kufanya mazungumzo na Marekani kwa hakika ni agizo kwa Serikali na lazima lifuatwe na kutekelezwa katika uwanja wa siasa na diplomasia.

Kulingana na Shirika la Habari la Hawza, maandiko ya taarifa ya Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Wilayat _ Al-Faqih (Mamlaka ya Faqih) katika uongozi wa jamii ya Kiislamu na usimamizi wa masuala ya kijamii ya Taifa la Kiislamu katika kila zama na kila wakati ni mwendelezo wa Wilayat / Mamlaka ya Kinabii na Alawi (Amani iwe juu yao).

Nuru hii ya Mwongozo / Uongofu umeiepusha Dini na Nchi kutoka katika upotofu na uharibifu kwa miaka mingi, na leo hii, kutokana na turathi hiyo adhimu, Iran ndiyo nchi pekee inayosonga mbele kuelekea kwenye ustaarabu wa Kiislamu.

Kauli za kistratijia na za kutafuta njia za Ayatollah al_Udhma Khamenei (Mwenyezi Mungu arefushe kivuli chake), alizitoa katika kikao na kundi la makamanda na wafanyakazi wa Jeshi la Anga na Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na ni onyo zito la Kiongozi huyu Muadhamu kuhusiana na tajriba chungu ya mazungumzo na Marekani yenye Kiburi na Uistikbari, na alishauri na kuthamini ijtihada na juhudi za Wizara ya Mashauri ya Kigeni katika Taifa la Iran, ambapo alisema:

“Hupaswi kujadiliana na Serikali ya namna hii, haina hekima, haina akili, haina heshima”. Kwa hakika hilo ni agizo kwa Serikali, na miongozo hii inapaswa kuzingatiwa na kutekelezwa katika nyanja ya siasa na diplomasia.

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, aliuita "Uzoefu" kuwa ni sababu bora ya kukaa mbali na mazungumzo na Marekani; Marekani, pamoja na rekodi yake ya ahadi mbaya na uovu, haipaswi kuwa na nafasi yoyote katika mfumo wetu wa maingiliano na maamuzi ya kitaifa, kikanda na kimataifa, na watu wote na Maafisa / Viongozi wa Iran wanapaswa kujua ukweli wa hila za vyombo vya habari, propaganda na madai ya ulaghai ya utawala huu wa kiburi na uistikbari.

Kiongozi Muadhamu alisema katika ibara yake dhidi ya adui:

"Wakitutishia, tutawatishia, na Ikiwa watatekeleza tishio hili, sisi pia tutatekeleza tishio hilo. Iwapo watashambulia usalama wa Taifa letu, tutashambulia pia usalama wao bila kusita."

Lazima tujue kwamba kujiondoa kutoka kwenye misingi na maadili ya Kiislamu na Kitaifa hakutaleta chochote kwa Taifa letu, na kufanya mazungumzo na adui wa dhahiri kama Marekani kunamaanisha kuingia katika mzunguko mbaya na usio na matunda.

Jumuiya ya Walimu ya Seminari ya Qom, ikisisitiza umuhimu wa maneno ya kuelimisha ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kuhusu mazungumzo na Marekani, inatangaza yafuatayo:

1- Kutatua matatizo ya nchi kunategemea mkono wenye nguvu wa vijana na utashi wa Kidini wa watu.

2- Vyombo vya Habari na wamiliki wa majukwaa ya Kisiasa wafuate mkondo wa ufafanuzi wa kauli hizi na kueleza hasara na madhara ya kuingia katika nara za kisiasa na hadaa za Wamarekani katika suala la maongezi na mazungumzo ya mapatano.

3- Marekani ni utawala wa kihalifu, utawala muovu, Utawala wenye uongo na usiokuwa mwaminifu, na kufanya mazungumzo na utawala kama huo kutasababisha hasara kamili na kurudi nyuma kwa nchi.

4- Marekani haijaacha juhudi zozote za kupunguza kasi ya harakati ya Taifa la Iran, na bila shaka mchezo wa mazungumzo ya mapatano ni uongo wa wazi wa kupunguza nguvu na uwezo wetu. Hakuna mtu anayekataa uwepo wa matatizo.

Matabaka tofauti ya watu wana matatizo; Lakini jambo linalotatua matatizo haya ni jambo la ndani, ambalo ni “Juhudi za Viongozi wanaojitolea na kuungwa mkono na Taifa la Umoja”; Viongozi na Maafisa wanapaswa kujua kwamba ili kutatua matatizo, mtu anapaswa kuamini nguvu na uwezo wa ndani na kutumia uwezo wote kushinda vikwazo.

5- Maandamano ya Watu tarehe 22 Bahman (Februari 10, 2025); Maadhimisho ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambayo ni dhihirisho la Umoja wa Kitaifa nchini na kujifunza kutoka kwa Qur'an Tukufu na maamrisho ya Uislamu mpendwa, yanaonyesha azma ya Taifa na Serikali ya kutatua matatizo ya Jamii na kufifisha njama za adui, na itawaangusha wenye kiburi na uistikbari katika kufikia malengo yao maovu kuelekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tunatumaini kwamba Mwenyezi Mungu atatufanikisha katika kutimiza wajibu wetu.

Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha

Comments

  • Hatibu Nkonga TZ 14:22 - 2025/02/09
    We agree 👍